MWIMBAJI na rais wa Mashujaa Band, Chaz Baba Jumamosi iliyopita alipanda jukwaa la Extra Bongo kusalimia kisanii na kukonga nyoyo za mashabiki wa bendi hiyo.
Hiyo ilikuwa ndani ya ukumbi wa Meeda Club, Chaz Baba akajumuika na Extra Bongo kuimba wimbo "Regina Zanzibar" watu wakapagawa na kuhamasika kwenda kumtunza pesa kibao.
Baada ya wimbo huo Chaz Baba akasema: "Ally Chocky ni kaka yangu, namheshimu sana, nimepita kumsalimia kama hivi, amenipa fursa ya kupanda kidogo Napata pesa ya mafuta."
Comments
Post a Comment