HUU ni msiba mwingine mkubwa, tene pengine ni msiba mkubwa zaidi. Producer, Director na mwandishi wa filamu pamoja na tamthilia, George Tyson amefariki kwa ajali ya gari.
Habari zilizoifikia Saluti5 zinasema Tyson alikuwa akitokea Dodoma kurejea Dar es Salaam na ndipo akapata ajali hiyo.
Tyson ndiye mtu aliyeleta mapinduzi ya tahmthilia hapa nchini, lakini pia akafanya mageuzi katika filamu kwa kuitoa kwenye kuuza sura hadi kuwa biashara. Alishiriki katika kuandaa filamu ya Girlfriend iliyoleta mapinduzi makubwa.
Habari zaidi zitakujia baadae.
Comments
Post a Comment