Benki ya posta YAZINDUA KADI ZA AKAUNTI KWA WANACHAMA NA MASHABIKI wa SIMBA NA YANGA



benki ya posta YAZINDUA KADI ZA AKAUNTI KWA WANACHAMA NA MASHABIKI wa SIMBA NA YANGA
 Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa Simba waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam
 Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi mtangazaji Ephraim Kibonde wa Clouds FM mfano wa kadi ya akaunti ya benki hiyo hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni msemaji wa Simba Bi Asha Muhaji na kulia ni Afisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Bw. Kamwaga
  Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi mmoja wa mashabiki wa Yanga  kadi ya akaunti ya benki hiyo hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni msemaji wa Simba Bi Asha Muhaji na kulia ni Afisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Bw. Kamwaga
 Kadi ya akaunti ya Benki ya Posta kwa mwanachama wa Yanga, ambapo wao wameanza na wanachama kufungua akaunti na kupata kadi hii, na baada ya miezi mitatu mashabiki watafanya hivyo
  Kadi ya akaunti ya Benki ya Posta kwa mwanachama wa Simba. Tofauti na Yanga kadi za Simba zitaanza kugawiwa kwa mashabiki ambao watafungua akaunti, na baada ya miezi mitatu wanachama watapata fursa hiyo. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii.



Comments