ARSENE Wenger amekiri kuwa yupo tayari kumwaga pesa kwa fujo kwenye usajili kiangazi hiki ili kuitengeneza upya Arsenal na kuifanya iwe mgombea wa ukweli wa taji la Ligi Kuu.
Hiyo imekuja baada ya kocha huyo kusaini mkataba mpya wa kuikochi Arsenal kwa miaka mitatu zaidi – mkataba wenye thamani ya pauni milioni 8 kwa msimu.
Arsenal itamkabidhi Wenger pauni milioni 100 kwaajili ya kufanya usajili wa nguvu huku ikiaminika kuwa nguvu yake kubwa ameilekeza kwa nyota wa Real Madrid Karim Benzema na Alvaro Morata, Mario Mandzukic wa Bayern Munich na Loic Remy wa Newcastle.
Comments
Post a Comment