AUDIO: MUUMIN AISHUTUMU VIKALI BENDI YA JAMBO SURVIVORS … kisa? Mazishi ya Amina Ngaluma, asema mwili wake umeletwa kama kiroba cha mahindi, ailalamikia pia Bongo Movie, amshangaa Nyoshi



AUDIO: MUUMIN AISHUTUMU VIKALI BENDI YA JAMBO SURVIVORS … kisa? Mazishi ya Amina Ngaluma, asema mwili wake umeletwa kama kiroba cha mahindi, ailalamikia pia Bongo Movie, amshangaa Nyoshi
AUDIO: MUUMIN AISHUTUMU VIKALI BENDI YA JAMBO SURVIVORS …            kisa? Mazishi ya Amina Ngaluma, asema mwili wake umeletwa kama            kiroba cha mahindi, ailalamikia pia Bongo Movie, amshangaa            Nyoshi

MWIMBAJI nyota wa dansi Mwinjuma Muumin amesema amekerwa na bendi ya Jambo Survivors iliyoko Thailand aliyokuwa anaitumikia marehemu Amina Ngaluma, kwa kushindwa kutuma mwakilishi yeyote katika mazishi.

Jambo Survivors ni bendi inayoundwa na Watanzania ikiongozwa na mpiga kinanda Hassan Shaw.

Akiongea na kituo cha radio cha East Africa jana usiku, Muumin alisema  bendi hiyo imeonyesha ubabaishaji mkubwa katika suala zima la mazishi ya Amina Ngaluma. Utamsikiliza mwenyewe mwishoni mwa habari hii.

"Wametoa taarifa ya ubabaishaji, eti wamekosa booking ya ndege, siku 9 unakosaje tiketi?," alihoji Muumin.

"Baadae wakatoa taarifa nyingine kuwa wameshindwa kuja kwasababu ya utata wa tajiri yao ambaye anawataka waanze kazi tarehe 24 kwa sababu siku walizokaa bila kufanya kazi ni nyingi. Tarehe 24 ndiyo siku ya kuzikwa Amina, wanawezaje kufanya kazi siku kama hiyo?" alisikitika  Muumin na kuongeza: "Wametuletea Amina Ngaluma kama kiroba cha mahindi".

Muumin pia amemshangaa Nyoshi kushiriki mazishi ya msanii wa Bongo Movie, Adam Kuambiana huku akishindwa kushiriki mazishi ya mwanamuziki mwenzake.

Akizungumzia wasanii wa Bongo Movie, Muumin alisema wanamuziki wa dansi wamekuwa washiriki wakubwa wa wasanii wa filamu lakini wao hawafiki kwenye mazishi ya wanamuziki wa dansi.

"Msanii pekee wa Bongo Movie niliyemuona maburini ni Dr Cheni, tena huyu amekuja kwa kuwa alikuwa MC kwenye harusi ya Amina Ngaluma na Rashid Sumuni," alifafanua Muumin. (Saluti5 inachukua nafasi hii kumfahamisha Muumin katika mazishi ya Amina, walikuwepo pia Chiki Mchoma na mchekeshaji Pembe).

Muumin pia ameishangaa TOT kutotuma mwakilishi hata mmoja wakati marehemu alifanya kazi hapo. "Nilimuona Ali Jay tu (akimaanisha msanii msaatafu wa TOT, Juma Jerry "JJ Mzee wa Mbezi), ambaye alikuja kwa niaba yake mwenyewe," alilalamika Muumin ambaye yeye pamoja na mume wa marehemu, waliwahi pia kuitumikia TOT.

Kilichoandikwa hapa ni kidogo sana, msikilize Muumin hapo chini akipasuka zaidi kupitia East Africa Radio, kwa hakika utapata mengi sana.



Comments