AUDIO: MSIKILIZE MUUMIN ALIVYONGURUMA EAST AFRICA RADIO, ATAKA CHAMUDATA WAPISHE DAMU MPYA

AUDIO: MSIKILIZE MUUMIN ALIVYONGURUMA EAST AFRICA RADIO, ATAKA CHAMUDATA WAPISHE DAMU MPYA
AUDIO: MSIKILIZE MUUMIN ALIVYONGURUMA EAST AFRICA RADIO,            ATAKA CHAMUDATA WAPISHE DAMU MPYA

MWINJUMA Muumin (mwenye kofia pichani) amewataka viongozi wa Chama Cha Muziki Tanzania wakae kando na kupisha damu mpya kwa vile wao kazi imewashinda.

Akiongea live jana usiku kupitia kituo cha radio cha East Africa, Muumin alionyesha kusikitishwa kwake na jinsi chama hicho kilivyoshiriki mazishi ya mwimbaji Amina Ngaluma.

Mwimbaji huyo aliyefanyakazi na Amina Ngaluma kwa muda mrefu alishangaa kitendo cha Mwenyekiti wa Chamudata kuzungumzia mambo ya kung'anywa ofisi katika kikao cha maandalizi ya mazishi ya Amina Ngaluma kilichofanyika Vijana Social Hall siku ya Alhamisi.

"Yaani tuko kwenye kikao cha maandalizi ya mazishi, tunachangishana halafu mtu anaingiza habari ya kunyang'anywa ofisi. Hapo ndipo unaposhangaa mtu ana upeo wa namna gani," alisema Muumin.

Muumin ameongea jambo hili kwa kirefu na kwa kina hebu msikilize hapo chini, jitahidi upate muda wa kuisikiliza 'clip' hii.

Comments