HATIMAYE lile bifu kali la Asha Baraka na Ally Chocky limefikia ukingoni na wiki hii watakalishwa meza moja na kuzika rasmi tofauti zao. Mwishoni mwa habari hii utaisikia sauti ya Chocky ikitoa ufafanuzi.
Saluti5 imepenyezewa za chini ya zulia kutoka watu wa ndani wa pande zote mbili (Asha Baraka na Choky) kuwa juhudi za kupatanishwa kwao zilianza wiki mbili zilizopita na sasa ziko katika hatu nzuri.
Imeelezwa kuwa kampuni moja kubwa ya uchapishaji magazeti, ndiyo imebeba dhima ya kumaliza bifu la Chocky na Asha Baraka ambapo leo Jumatatu wote wawili watakutanishwa watakutanishwa meza moja.
Asha Baraka na Chocky ilikuwa wakutanishwe Ijumaa iliyopita, lakini pilika za maandalizi ya mazishi ya Amina Ngaluma, zikasogeza mbele kikao hicho cha usuluhishi.
Bifu la Asha Baraka na Chocky lilikolea mara baada ya Ally Chocky kuongea na Saluti5 na kusema iwapo atafariki basi Asha Baraka asimzike.
Habari hiyo ikawa kubwa na kunakililwa na blogs nyingi pamoja na magazeti kibao na kuanzia hapo watu hao wawili wakawa paka na panya. Hata majuzi kwenye kikao cha maandalizi ya mazishi ya Amina Ngaluma, wawili hao walipishana kama hawajuani.
Chocky alipoulizwa kama ni kweli kuna juhudi za kupatanishwa akasema: "Juhudi zipo na mimi binafsi nimekunjua moyo wangu, nadhani ni muhimu kusameheana.
"Nimesamhe aliyonikosea na yeye pia kama yapo niliyomkosea basi ni vema akasamehe."
Sikiliza sauti ya Ally Chocky kama alivyorekodiwa na Saluti5.
Comments
Post a Comment