ARSENAL imefufua tena mbio za kumnasa kiungo wa Ujerumani Sami Khedira anayekipiga Real Madrid.
Arsene Wenger alijaribu kumsaini kiungo huyo katika dirisha la usajili la Januari lakini mchezaji huyo aliyeumia goti mwezi Oktoba, akabainika kuwa jeraha lake ni kubwa zaidi kuliko ilivyofikiriwa.
Khedira, 27 ndio kwanza amerejea uwanjani na sasa Wenger anaona kumsajili kiungo huyo ni rahisi zaidi kuliko kumsajili upya nyota wake wa zamani Cesc Fabregas.
Wakati Arsenal watalazimika kulipa pauni milioni 30 kwa Barcelona kwaajili ya Fabregas, Khedira aliyebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake atamgharimu Wenger pauni milioni 15 tu.
Comments
Post a Comment