LEO NI MIAKA 11 TANGU AFARIKI SULEIMAN MBWEMBWE



LEO NI MIAKA 11 TANGU AFARIKI SULEIMAN MBWEMBWE

Tarehe kama ya leo miaka 11 iliyopita (12/6/2004) Tanzania ilipoteza mmoja wa waimbaji bora kabisa kupata kutokea katika muziki wa dansi – Suleiman Mbwembwe.
Marehemu Suleiman Mbwembwe (pichani kushoto) katika uhai wake alitamba zaidi na bendi za Msondo Ngoma na Vijana Jazz na moja ya tungo zake za kutukuka zitakazodumu milele na milele ni "Prisila" alioutunga na kuimba kupitia Msondo Ngoma katikati mwa miaka ya 80.
Hadi anafariki, Mbwembwe alikuwa ni mwimbaji wa Msondo Ngoma ambapo kifo chake kinaunda pengo la waimbaji mabingwa wa bendi hiyo waliotangulia mbele ya haki ndani kipindi hicho cha miaka 11 wakiwemo Athuman Momba, TX Moshi William, Joseph Maina na Muhidin Maalim Gurumo.
Shukran za dhati kwako mdau Senetor Mwinyi kwa kutukumbusha siku hii muhimu.


Comments