COASTAL, AZAM ZAENDELEZA USHINDI



COASTAL, AZAM ZAENDELEZA USHINDI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYoTp2udHNs2JHo74GJ2vwTh4MoK3S5P0rnViRi94assSQ_q4DYGC2pETRg039r5Af76IbN4qoMRo4ke-zN6Bd3YDhznrBccnvstPYBbPlVjPiIoBRuUmvPSYnqh2dquq4ffi2-6khiEE/s1600/AGGREY+BAO.jpg
Mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC leo wameendeleza ubabe wao kkwa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine baada ya kuichapa goli 1-0 na kuwa mchezo wa 38 wa ligi kuu ya vodacom wakicheza bila ya kupoteza.

Katika mchezo huo ulioanza saa kumi na nusu goli la Azam FC lilipatikana katika dakika ya 23 kupitia kwa Beki Aggrey Morrice akipiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja hadi kwenye nyavu za Mbeya city.

Kabla ya Mchezo wa leo Mbeya city walikuwa hawajapoteza mchezo wowote ule wala kuruhusu nyavu zao kuguswa katika michezo mitatu ya wali ambapo walitoka suluhu na JKT Ruvu kabla ya kuwafunga Coastal union goli 1-0 na kisha kutoka suluhu na Ruvu shooting.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, Coastal union wamefanikiwa kuvuna pointi 3 baada ya kuwachapa goli 2-0 Mgambo shooting na kupelekea kufikisha pointi 7 katika michezo minne aliyo cheza.


Magoli ya Coastal union katika mchezo wa leo yamefungwa na Ramadhan Salim katika dakia ya 35 na Kenneth Masumbuko katika dakika ya 90.


Ushindi huo wa leo ni wa pili mfululizao kwa Coastal Union ambayo inamikakati ya kurejesha makali yake ya mwaka 1988.

Comments