BAADA ya kushindwa kuiwakilisha Brazil kwenye michuano ya Copa America, nyota Neymar atakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki ya mwaka huu.
Kocha wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, Rogerio Micale ndie anayekiongoza kikosi hicho kwa sasa baada kutupiwa virago.
Katika kikosi chake ambacho kimejengwa na idadi kubwa ya damu changa, Mikale pia amemjumuisha staa wa Bayern Munich, Douglas Costa.
Wachezaji pekee wanaoonekana kuwa na umri mkubwa ni, Costa, Neymar na mlinda mlango wa klabu ya Palmeires, Fernando Prass.
Pia kocha huyo amemwita kikosini kinda Gabriel Barbosa ambaye mwezi uliopita alifunga bao lake la kwanza katika michuano ya kimataifa.

Comments
Post a Comment