NI hofu tupu… Chelsea imeripotiwa kuhofia kukimbiwa na mastaa wake wanne msimu huu baada ya kufeli kufuzu kucheza Champions League msimu ujao.
Matumaini ya kweli kwa Chelsea kufuzu Champions League msimu ujao ni kushinda taji la michuano hiyo msimu huu.
Chelsea inashika nafasi ya 12 katika Premier League, ikiachwa pointi 14 na Manchester City iiliyo juu ya mstari wa kugawa timu za 'Top Four' wakati zikibaki mechi 12 kumaliza msimu.
Timu hiyo ya Stamford Bridge ilimtupia virago Jose Mourinho Desemba mwaka jana na ikarudi kwenye chati chini ya Guus Hiddink ambaye hajapoteza mechi katika ligi, lakini juhudi zake hazipewi nafasi ya kuzuia mastaa wasiondoke kiangazi hiki.
Kwa mujibu wa gazeti la The Times, mastaa wanne wanaotarajiwa kutimkia katika timu zenye nafasi ya kucheza Champions League ni Eden Hazard, Thibaut Courtois na Diego Costa huku John Terry akiwa tayari amethibitisha kuondoka.
Comments
Post a Comment