STAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amedai kuwa            anajua ni kwanini Lionel Messi aliamua kupiga penalti kwa            kumpasia Luis Suarez aliyefunga katika mechi ya La Liga dhidi            ya Celta Vigo Jumapili iliyopita, lakini amekataa kuweka wazi            kwa vyombo vya habari.
        Ronaldo alifumba fumbo hilo katika mkutano na waandishi            wa habari kuelekea mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya            hatua ya 16 bora, alipoulizwa kuhusu 'pasi ya penalti ya Messi            kwa Suarez' iliyotawala vyombo vya habari.
        "Najua kwanini alifanya hivi, lakini sina cha ziada cha            kuongeza," alisema Ronaldo mwenye umri wa miaka 31 na kuwaacha            wanahabari 'kwenye mataa' wakihangaika kujiuliza            alichomaanisha.
        Katika kutafuta              alichomaanisha Ronaldo, baadhi waliona            ni katika kuonyesha heshima kwagwiji            Johan Cruyff, ambaye              alifanyatukio kama hilo enzi zake akiichezea Ajax            mwaka 1982, wakati wengine wanadhani Messi            alikuwa akimsaidia Suarez            kumkimbia Ronaldo katika mbio za            kuwania tuzo ya mfungaji bora wa La Liga - Pichichi.
        Pasi hiyo ya penalti katika mechi waliyoshinda 6-1            ilimfanya Suarez kukamilisha 'hat-trick' na kufikisha mabao 23            mbele ya Ronaldo aliyebaki na mabao 21. Messi ana mabao 13            katika msimamo huo.
        
Comments
Post a Comment