Manchester United itafanya mazungumzo na kocha Louis van Gaal mwanzoni mwa mwaka mpya ili kuangalia uwezekano wa Mdachi huyo kusaini mkataba mpya Old Trafford.
Licha ya kushutumiwa kwa soka bovu la Manchester United chini yake sambamba na tishio la kung'olewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku, wamiliki wa klabu hiyo pamoja na makamu mtendaji mkuu Ed Woodward, wanafurahia maendeleo yaliyoletwa na Van Gaal tangu achukue timu miezi 17 iliyopita.
Mkataba wa sasa wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, unatarajiwa kumalizika katikati ya mwaka 2017 na sasa United imeamua kufungua milango ya kurefusha mkataba huo.
United inatarajiwa kuweka wazi mwelekeo wa hatma ya Van Gaal ndani ya miezi michache ijayo na tayari wako na mikakati mipya kwaajili ya msimu ujao.
Mikakati hiyo itaipa Manchester United miezi 12 ya kutafuta mbadala wa Van Gaal iwapo ataamua kuondoka Old Trafford.
Bodi ya Manchester United haitaki majanga ya kusaka kocha mpya kwa kukurupuka kama ilivyotokea baada Sir Alex Ferguson kustaafu ghafla mwaka 2013.
Bodi ya Manchester United haitaki majanga ya kusaka kocha mpya kwa kukurupuka kama ilivyotokea baada Sir Alex Ferguson kustaafu ghafla mwaka 2013.
Hapo awali Van Gaal alisisitiza kuwa hiki ni kibarua chake cha mwisho katika soka na anatarajiwa kuachana na kazi ya ukocha mara tu mkataba wake wa miaka mitatu United utakapomalizika ili kulinda ahadi aliyompa mkewe Truus.
Manchester United inatarajiwa kufanya mazungumzo na Louis van Gaal kwaajili ya mkataba mpya
Licha ya shutuma nyingi juu yake lakini Van Gaal bado ni lulu kwa bodi ya Manchester United
Comments
Post a Comment