Kasi ya klabu ya FC Barcelona jumamosi ya wiki iliyopita ilipigwa 'stop' na Valencia, huku rekodi zao kadhaa zikivunjwa baada ya matokeo ya sare 1-1 katika uwanja wa Mestalla.
Moja ya rekodi za Barca zilizovunjwa kutokana na sare vs Valencia, ni ngome yao kuruhusu goli baada ya dakika takribani 526 katika ligi kuu ya Uhispania, goli lilofungwa na Santi Mina – kinda wa miaka 19 na siku 363, mchezaji mdogo zaidi kuifunga Barcelona goli tangu Sergio Aguero alipoifunga akiwa na miaka 19 mnamo mwaka 2008.
Pamoja na rekodi hizo lakini kubwa kuliko ni kuvunjwa kwa rekodi iliyodumu kwa miaka 14, ya kucheza mechi nzima bila kufanya substitution yoyote katika mechi ya La Liga.
Luis Enrique aliwashangaza wengi kwa kuamua kutofanya mabadiliko yoyote katika kikosi kwenye huo. Marc-André Ter Stegen, Marc Bartra, Munir, Sandro, Adriano, Thomas Vermaelen na Sergi Samper wote walibaki kwenye benchi kwa dakika zote 90.
Mara ya mwisho kwa kocha wa Barcelona kuamua kucheza mechi nzima bila kufanya mabadiliko – ilikuwa msimu wa 1998/99 wakati Louis van Gaal alipoamua kucheza mechi nzima bila kumtumia mchezaji yoyote kutoka kwenye benchi.
Comments
Post a Comment