HATA kama miamba ya soka England, Mnchester United wameshaanza kufanya maongezi na Marko Grujic, lakini ni Chelsea ndio ambayo imedaiwa kufika bei kwa nyota huyo wa Serbia.
Gazeti la michezo la Italia, 'Gazzetta dello sport' jana limeandika habari, Chelsea imeshapeleka posa kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, kwa aili ya kuitumikia klabu hiyo inayopepesuka katika msimu huu wa Ligi Kuu.
Grujic ameonyesha uwezo mkubwa katika kikosi cha Red Star Belgrade msimu huu kiasi cha kuzivutia klabu kubwa, ikiwamo Man United.
Mkataba wa mchezaji huyo katika kikosi cha timu hiyo ya Serbia unakoma mwaka 2018 lakini Belgade wanaweza kuongea na klabu yoyote kwa ajili ya kufanya biashara.
Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la nchini Serbia, liitwalo Vecernje Novost, Manchester United walifanya mazungumzo na mchezaji huyo baada ya kuona makali yake wakati anacheza katika kikosi cha timu ya taifa ya Serbia chini ya miaka 21, dhidi ya wenzao wa Italia Ijumaa.
Lakini imeandikwa pia na Gazzetta kwamba miamba wengine wa Ligi ya Serie A ya Italia, klabu ya Inter Milan pia wamepeleka ofa ya Euro mil. 2, huku Chelsea wakipandisha dau hilo mara mbili na kufikia Euro mil 4.
Ni kutokana na uwezekano huo, Chelsea wamepewa umuhimu mkubwa wa kumsajili mchezaji uyo na kufuta kabisa ndoto za Manchester United kumsajili wao.

Comments
Post a Comment