MANCHESTER UNITED inaonekana kukaribia            kumnasa Sergio Ramos baada ya klabu yake ya Real Madrid kutupa            ndoano kwa Leonardo Bonucci wa Juventus, anayetajwa kuwa            mbadala sahihi wa sentahafu huyo.
        Ramos mwenye umri wa miaka 29, anaonekana            kuwa njiani kuondoka Madrid kiangazi hiki, huku Louis van Gaal            akipambana kwa nguvu zote kupata saini yake, na tayari ameweka            mezani ofa ya pauni milioni 49.6.
        Kwa mujibu wa mtandao wa Tuttomercatoweb,            Real Madrid imeridhia kumwachi Ramos aondoke wakati ikielekeza            macho yake kwa Bonucci.
        
Comments
Post a Comment