MORGAN SCHNEIDERLIN HUYOOO OLD TRAFFORD, KUTUA MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MIL 25 ...Arsenal, Tottenham imekula kwao



MORGAN SCHNEIDERLIN HUYOOO OLD TRAFFORD, KUTUA MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MIL 25 ...Arsenal, Tottenham imekula kwao

Manchester United ni kama imeshafanikiwa kumsajili kiungo wa kutakata wa Southampton Morgan Schneiderlin kwa pauni milioni 25.
Southampton imekubali ofa ya pauni milioni 20 ya Manchester United na zitaongezeka pauni milioni 5 hapo baadae kutegemea maendeleo ya mchezaji huyo yatakavyokuwa Old Trafford.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amethibitisha safari yake ya United kwa kusema: "Nashukuru sana mazungumzo ya usajili wa Manchester United yanaendelea vizuri na yatakamilika hivi karibuni."
United imekuwa ikimsaka Schneiderlin kwa zaidi ya miezi sita na usajili wake utafutilia mbali uwezekano wa kiungo wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger kutua Old Trafford.
Schneiderlin, 25, alikuwa pia akifukiziwa na Arsenal na Tottenham lakini akaifanya United kuwa chaguo lake la kwanza.
Southampton walimpa ofa mpya ya pauni 60,000 kwa wiki lakini akaikataa na sasa United wanatagemea kumlipa mara mbili yake - pauni 120,000 kwa wiki. 
SAFARI IMEWADIA: Man United inaelekea kushinda mbio za kumsajili Morgan Schneiderlin 
Van Gaal anaamini Schneiderlin anaweza akazungusha vizuri  kwenye eneo la katikati ya uwanja na kuleta ushindani kwa Michael Carrick.


Comments