KUISHUHUDIA MALAIKA BAND SASA LAZIMA UVUNJE KIBUBU …yaweka rekodi mpya ya kiingilio Mango Garden



KUISHUHUDIA MALAIKA BAND SASA LAZIMA UVUNJE KIBUBU …yaweka rekodi mpya ya kiingilio Mango Garden
KUISHUHUDIA MALAIKA BAND SASA LAZIMA UVUNJE KIBUBU            …yaweka rekodi mpya ya kiingilio Mango Garden

Malaika Band sasa iko matawi ya juu na ili kushuhudia onyesho lao, mshabiki atalazimika kulipa kiingilio cha shilingi elfu kumi.

Rais bendi hivyo, Christian Bella ameiambia Saluti5 kuwa kiingilio katika maonyesho yao kila Ijumaa hapo Mango Garden kitakuwa buku 1o.

Bella ameongeza kuwa hata baadhi ya maonyesho yao mengine watakayoandaa wao kama bendi kwenye kumbi zingine, kiingilio kitakuwa shilingi elfu 10, ila kwa yale yatakayoandaliwa na mapromota, bei inaweza kupungua kutokana na utashi wa promota.

Pamoja na ukubwa wa bei, Bella amewaahidi mashabiki wa bendi hiyo kuwa watapata burudani ya nguvu itakayolingana na thamani ya pesa yao.

Kiingilio cha shilingi elfu kumi kwa maonyesho ya kila wiki Mango Garden (ukiondoa maonyesho maalum ya mlipuko), kinakuwa ni rekodi mpya. Hakuna bendi yoyote inayopiga hapo kila wiki kwa kiingilio kama hicho.

Makundi yote yaliyokuwa na yale yanaoendelea  kuwa na maskani Mango Garden kama vile Twanga Pepeta, Akudo, Jahazi na Mashauzi Classic hayajawahi kuwa na kiingilio kama hicho kwa kila wiki labda tu katika maonyesho maalum au show za sikukuu.

Je Malaika Band watamudu kudumu na kiingilio hicho au watasalimu amri mbele ya safari? ni jambo la kusubiri.



Comments