TANZANIA YAINGIZA WAAMUZI 11 WAPYA KWENYE ORODHA YA FIFA.



TANZANIA YAINGIZA WAAMUZI 11 WAPYA KWENYE ORODHA YA FIFA.

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua ulimwenguni,
Kwenye orodha hiyo kuna jumla ya waamuzi 18 kutoka nchini Tanzania,miongoni mwa waamuzi hao wapo 11 wapya pamoja na 7 wa zamani.
NKONGOO
Waamuzi wapya wa kati kwenye orodha hiyo kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro,kwenye orodha hiyo mpya pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail.
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wapya kwenye orodha hiyo wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila wakati kwa upande wa wanawake wasidizi ni Kudura Omary Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala.
Majina ya wamuzi wa zamani yaliyoka tena kwenye orodha hiyo ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali,Fernand Chacha,John Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu .
nkongo



Comments