MWANAMUZIKI WA SIKU NYINGI ISSA NUNDU AFARIKI KCMC MOSHI



MWANAMUZIKI WA SIKU NYINGI ISSA NUNDU AFARIKI KCMC MOSHI

Mwanamuziki muimbaji wa siku nyingi ambaye amewahi kuimbia bendi nyingi zikiwemo Maquis, MK Group ,Makassy, Wazee Sugu amefariki jana alfajiri katika hospitali ya KCMC Moshi.

Issa ambaye alianza kuugua muda mrefu na kukutwa anatatizo la kusinyaa ubongo, aliamua kurudi kwao Kongo lakini alipofika Kigoma alizidiwa na kulazwa huko ambako alihamishiwa KCMC Moshi kwa matibabu zaidi. Issa ambaye jina lake halisi ni Jackson Issa Nundu atazikwa Moshi siku ya Jumanne ikiwa taratibu zote zitakamilika. Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa,

Mungu amuweke pema peponi JAckson Issa Nundu

index

Kasongo Mpinda na Marehemu Issa Nundu

maquis dodoma

Issa Nundu wa pili toka kushoto mwenye suruali nyeusi hapa wakiwa na Mquis katika uwanja wa Jamhuri Dodoma



Comments