MANCHESTER UNITED SASA WAELEKEZA NGUVU ZOTE KWA DI MARIA NA KHEDIRA … Ed Woodward aahidi kufanya usajili wa kishindo



MANCHESTER UNITED SASA WAELEKEZA NGUVU ZOTE KWA DI MARIA NA KHEDIRA … Ed Woodward aahidi kufanya usajili wa kishindo

Pair of aces: Angel Di Maria (left) and Sami                    Khedira are both on Manchester United's radar

MANCHESTER United inajiandaa kupeleka ofa ya kumnasa winga anayetaka kutimka Real Madrid, Angel Di Maria pamoja na mchezaji mwenzake Sami Khedira.

Habari njema kwa mashabiki wa United ni kwamba mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward ameahidi kusajili wachezaji wengine wawili kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti alisema Alhamisi kuwa Di Maria na Khedira wanaweza kuondoka. Di Maria amekuwa akiwindwa na boss wa United Louis van Gaal kwa dirisha lote hili la usajili, lakini pia anamjua vilivyo Khedira tangu alipokuwa Ujerumani.

Ancelotti alisema: "Kama Di Maria hatapata suluhisho la hatma yake, tutafurahi kumkaribisha tena kikosini pale diirisha litakapofungwa.

"Ameomba kuondoka, hajakubaliana na mapendekezo ya mkataba mpya. Ni mchezaji wa Real Madrid hadi August 31, kama ambavyo nimewahi kusema, chochote kinaweza kutokea.

"Suala la Khedira lipo tofauti. Hajaomba kuondoka. Amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya, lakini bado ana mwaka mmoja wa mkataba wake. Tutaona kitakachotokea."

Usajili huo utakuwa ni tulizo kwa mashabiki wa United ambao wamekuwa wakionyesha hasira zao kwa klabu kushindwa kufanya usajili wa maana na wamedhamiria kufanya maandamano katika mechi dhidi ya QPR mwezi ujao.



Comments