HATIMAYE yametimia. Wakati mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward aliposema kuwa watavunja rekodi ya usajili England msimu huu, ilionekana kama masihara lakini sasa ukweli umedhihirika.
Angel di Maria tayari ametua Manchester United kwaajili ya mazungumzo binafsi pamoja na vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 60 utakaomwingizia mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
Di Maria ameonekana kwenye gari akiwa ameketi kiti cha nyuma akielekea kwenye uwanja wa mazoezi wa United kwaajili ya kwenda kukamilisha usajili wake.
Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa pesa nyingi zaidi Manchester United akitanguliwa na Wayne Rooney na akiwa amemzidi kidogo Robin van Persie.
Comments
Post a Comment